top of page

Nasikia Kelele na Vigelegele

Nasikia kelele na vigelegele nauliza

kwani kuna nini (leo). Nawaona walio

na mavazi mazuri wanavyotembea kwa

mariongo tele (leo).


Ni harusi pigeni kelele. Ni harusi pigeni

makofi. Ni harusi tuimbe kwa shangwe,

na vigelegele tupige x2.


Tazameni bwana anavyopendeza,

anavyokanyanga polepole (sana).

Naye bibi harusi anametameta,

anapambwa mavazi mazuri (sana).


Nyanyueni bendera mikononi mwenu

muzipeperushe kwa pamoja (wote).

Simameni tucheze kwa furaha,

wanapoingia, tuimbe kwa shangwe (wote).


Tuwafurahieni ndugu zetu hawa

walioamua kufunga (ndoa).

Ndoa ni maagizo yake Mungu Baba

kwa upendo wasivunje hiyo (ndoa).


Ewe bwana harusi umpende mke wako

siku zote umlinde (vyema).

Naye bibi harusi mheshimu mume wako

siku zote umtunze (vyema).

15 views0 comments

Comentarios

Obtuvo 0 de 5 estrellas.
Aún no hay calificaciones

Agrega una calificación
bottom of page