top of page

Naomba Baraka


Kama ulivyo wingi wa nyota za angani ninaomba Bwana uyajaze Baraka maishayangu x2 (Neema zinitiririkie rehema zinitiririkie naomba furaha yako Bwana naombafaraja yako Bwana, ninaomba Bwana uyajaze Baraka maisha yangu) x2


Kama ile Baraka uliyomjalia baba yetu mtumishi wako Abrahamu mfano wa nyota za angani mithili ya mchanga wa pwani naomba nijalie na mimi Baraka.


Na kamaYakobo na uzao wake wote Baraka zako uliujaza kwa upendo maana wewe una uweza na nguvu asili ya vyote naomba nijalie na mimi Baraka.


Unijaze nguvu na akili kiimani nahitaji mwanga na mwongozo wako Mungu daima uwe name Ee Bwana milele nikufuate wewenaomba nijalie na mimi Baraka.

90 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page