top of page

Nakushukuru Baba

1. Nakushukuru Baba, Baba Mwenyezi Mungu kwa kuwa umeniumba x 2

(Nitakulipa nini ee Mungu wangu chakukupendeza wewe) Baba mimi sina kitu chochote cha kulinganisha na ukarimu wako (Maombi yangu uyapokee na dua zangu zikufikie) kwa huruma yako Baba nisamehe mimi kwa makosa niliyoyatenda, tafadhali Baba uniongezee siku nyingi ili nikutumikie.

2. Nakutukuza Baba, wewe ni ngome yangu, ndiwe unayenilinda, pokea sifa Baba, sifa ni zako wewe Baba Mwenyezi Mungu

3. Nakuabudu Baba, Baba mlinzi wangu, kwa kuwa wewe ni mwema, uniongoze Baba, katika kweli zako, nifanye mapenzi yako.

4. Baba nifanye mimi, chombo cha kazi yako, nikutumikie wewe, pasipo na amani, pasipo na upendo nitangaze jina lako.

5. Usiniache Baba, uwe nami daima katika maisha yangu, nikufuate wewe, daima siku zote milele hata milele.

2 views0 comments

Comentarios

Obtuvo 0 de 5 estrellas.
Aún no hay calificaciones

Agrega una calificación
bottom of page