top of page

Nakuja Mbio Mbio


Nakuja kwako mbiombio nakuja kwako Mungu wangu Nilicho nacho mikononi ninakileta mbele zako (Pokea Baba sehemu ya mapato niliojaliwa Nakutolea ingawa ni kidogo sana kibariki.

Unipe nguvu na hekima niwe salama siku zote) x2


Nimekuja kwa shangwe kubwa nimejaa furaha tele Kwa vigelegele na nyimbo ninaleta sadaka yangu Nacheza cheza bila haya

bila hofu mbele zake Niliokabidhiwa bure inanipasa kweli nitoe bure.


Nimepata furushi langu kisha nitoe shukrani zangu. Bila wivu bila uchoyo ninakuja kukushukuru Nakuja bila dukuduku ninakuja kwa upendo. Nakuja kusema asante Mungu Baba kwa mema niliyopata.


Fedha zetu za mifukoni ninaleta kama sadaka.Mifugo ninaowafuga ninaleta kama zawadi.


Mavuno yote ya shambani ninaleta mbele zako, Ni matunda ya jasho langu ninakupa kwa moyo wa ukarimu.


Upokee mkate huu kutoka kwa zao la ngano Pokea na divai hii toka tunda la mzabibu Geuza mwili wake Yesu chakula cha Waumini, Geuza damu yake Yesu kinywaji chetu sisi tuaminio.


Moyo wangu uhai wangu mwili wangu ni mali yako. Nguvu zangu maisha yangu ninaleta ni mali yako Nakuja na unyenyekevu ninaomba shime yako, Naomba unipe fadhila, rehema na baraka za siku zote

8 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page