top of page

Naja Kwako Nipokee

Naja kwako nipokee ingawa mimi ni mdhambi x2

Sadaka naleta japo mi sifai,

Ewe Mungu Baba ipokee,

Mkate divai zao la mashamba,

Mbele yako Bwana twaleta.


Kazi zetu zote fedha zetu zote,

Mbele zako Bwana twaleta,

Nia zetu zote shida na furaha

Mbele yako Bwana twaleta.


Familia zetu kanisa na nchi,

Twazileta kwako ee Baba,

Twakuomba Baba utupe amani,

Imani pia na mapendo


Shukurani zetu tunakutolea,

Twakuomba Baba pokea,

Nazo nyoyo zetu nazo nia zetu,

Kwako Mungu Baba twaleta


Naja mbele yako ewe Mungu wangu,

huku nimejawa na dhambi.

Unihurumie uniwie radhi

mbele yako Baba natubu.

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page