top of page

Nainuka (Mimi) ninakwenda kwa Bwana (leo) napeleka(kile) alichonijalia, Mikononi (mwangu) nimebeba talanta (kweli) narudisha (ili) nikapate baraka x2

1. Mkate na divai Bwana upokee, ukageuze mwili na damu ya Yesu, fedha za mifukoni leo nimebeba mazao ya mashamba pia ninaleta

2. Mifugo nimefuga ninakutolea, nafaka nimevuna ninakutolea, kwa nguvu zako Baba nimefanya kazi, sehemu ya mapato yangu ninakupa

3. Umeniumba mimi kwa mfano wako, nakutolea nafsi yangu upokee, sina kitu kizuri cha kukutolea, pokea changu hiki japo ni kidogo

4. Ee Mungu Baba yetu unayo huruma, ututakase Baba kwa zawadi hizi, tufae mbele yako kutoa dhabiu, tukushukuru wewe daima milele

16 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page