top of page

Nahangaika hapa Duniani

1. Nahangaika hapa duniani, maisha yangu, hayana furaha, najua wazi hapa si nyumbani, bali njia ya kupita.

Niongoze vyema Maria mwema, bondeni huku niliko, nifike kwa usala, mbinguni kwa Yesu Mwanao x2.

2. Vita na shari vyote vyanisonga, mashaka mengi yananiijia, mwili na roho havina kinga, hatari imezidia.

3. Mama Maria ndiye jibu langu, hapa safarini unisaidie, uniombee kwa Mwanao Yesu, anikinge, anilinde.

4. Kwa kuwa Yesu ni Mwokozi wangu, nakusihi sana, nakusihi Mama, uzifikishe kwake shida zangu, unionee huruma.

17 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page