top of page

Mwanzi Uliopondeka


1. Utambi mchafu wa Moshi mzito, Hatauzima, kadhalika mwanzi, uliopondeka kamwe hatauvunja

(Hatanitupa), Bwana Yesu (milele yote) atanipigania, (Hataniacha) Bwana Yesu, (niangamie) atanipigania

2. Najua mtetezi wangu ni mwema, mwenye huruma, mwingi wa rehema, asiyeyahesabu maovu ya watu.

3. Nakiri Mimi mdhaifu kabisa, nimeanguka, kulitii neno, lakini nitamuangukia mwenyezi.

4. Nanyi ndugu zangu kweli, natubu. Niliyofanya, sikuwapendeza, nisameheni nichukulieni pia.


9 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page