top of page

Mungu Yule

  1. Nimemuona yule ninayemtafuta na neema zake, nimemuona leo nimemuona Mungu) x2. Mkononi mwake ana uzima tena ni wa milele, mkononi mwake ana uzima ninaoutafuta, na uzima huo anatoa bure kwa walio tayari, lakini kuna kanuni moja ya kwamba, uwajali watu.

  2. Nimemuona Mungu yu mtupu u hana nguo - anatamani mimi niende nikamvishe

  3. Nimemuona Mungu ana njaa hana chakula- anatamani mimi niende nikamlishe

  4. Nimemuona Mungu ni mgonjwa a kitandani- anatamani mimi niende kumtazama

  5. Nimemuona Mungu amefungwa a gerezani- anatamani mimi niende kumfariji

  6. Nimemuona Mungu ni mkimbizi mpakani- anatamani mimi niende kumpokea

  7. Nimemuona Mungu ni yatima hana wazazi- anatamani mimi niende nikamtunze

  8. Nimemuona Mungu ni mjane hana matunzo- anatamani mimi niende kumhifadhi

  9. Nimemuona Mungu amefiwa ana majonzi- anatamani mimi niende kumfariji

  10. Nimemuona Mungu ni kilema na hajiwezi- anatamani mimi niende kumuinua

  11. Nimemuona Mungu atolewa angali mimba- anatamani mimi niende kumtetea

  12. Nimemuona Mungu anapigwa kwa makombora- anatamani mimi niende suluhisha

  13. Nimemuona Mungu ni mtumwa ananyanyaswa- anatamani mimi niende kumtetea

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page