top of page

Mungu Wangu Mbona Umeniacha

Mungu wangu mbona umeniacha mimi Katika taabu zote hizi Maisha yangu ni ya mashaka Kwani sina raha nimekosa amani Matatizo mengi yananisonga (sana) Nakuomba Bwana nisaidie Maadui zangu wananiwinda (kutwa) Wanitega ili wanikamate Ninalala macho wazi mimi (kama ndege) Kama ndege mkiwa juu ya paa Nimekuwa kama mhuni mimi (fanya hima) Fanya hima Bwana kuniokoa

  1. Nimekuwa kama kichekesho kwa watu jamani mimi Bwana Kila nipitapo hunisema na kunicheka Wananizushia maneno ya uongo jamani mimi Bwana Mimi nimekuwa ni jalala la kila baya

  2. Maadui zangu kutwa wanisimanga jamani mimi Bwana Wananidhihaki wanisonya na kunitusi Jina langu limekuwa gumzo lao jamani mimi Bwana Sasa ndilo walitumialo kwa kulaania

  3. Na majivu yamekuwa chakula changu jamani mimi Bwana Na machozi yangu yamekuwa kinywaji changu Na siku zangu zinapita kama moshi jamani mimi Bwana Nakuomba usinichukue bado kijana

11 views0 comments

Commenti

Valutazione 0 stelle su 5.
Non ci sono ancora valutazioni

Aggiungi una valutazione
bottom of page