top of page

Mtakatifu Monica

Ee mama mtakatifu Monica ewe mlinzi wetu (wanao) Wewe ndiwe mwangaza wetu ewe malkia. Sisi wote twakusalimu (ee mama) Na kukupa zote heshima, kwa kuwa nasi wanao katika imani x2


Kila tunapokulilia wewe kweli husikia sauti yetu mama Hutuliza mioyo yetu na nafsi zetu hupata amani.


Ulikuwa mfano bora kwa wote walio na matatizo ya kijamii Ukaonyesha maombi na uvumilivu huleta umoja


Kwa maisha yako ya ukinaifu wakristu wote tupate mafunzo bora, Tuishi tukigawana Baraka tupatazo zote kwa furaha.


Sisi wana wa hii juia yako tunakuomba malkia utuongoze, Tuishi katika umoja, amani na upendo kutoka kwa Mungu.

5 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page