top of page

Mtakatifu Cecilia

Mtakatifu Cecilia utuombee, wewe ndiwe mwombezi wetu wa kwaya yetu

Siku ya leo twafurahia twakuimbia kwa furaha ee Cecilia x2


Tuonyeshe upole wako ee Cecilia, ili nasi tuwe wapole ee Cecilia

Utugawie imani yako tuwe na imani dhabiti kwa Mungu Baba x2


Tujalie tujitolee maisha yetu, kama ulivyojitolea kwa watu wote

Utuombee kwa Mungu Baba, tujitolee kwa wenzetu ee Cecilia x2


Katika kwaya tunaimba ee Cecilia, mara mia na tunacheza ee Cecilia

Utufadhili na sala zako, twakufurahia ee Mama wa kwaya yetu x2

3 views0 comments

Comentários

Avaliado com 0 de 5 estrelas.
Ainda sem avaliações

Adicione uma avaliação
bottom of page