top of page

Mshukuruni Mwokozi


Mshukuruni Mwokozi enyi mataifa, pigeni vigelegele pigeni makofi x 2

Tangazeni rehema zake hekaluni mwake, semeni ya kuwa Bwana ni mwenye adili x 2

  1. Njoni tumwimbie Bwana mwamba wa wokovu wetu, mikononi mwake zimo bonde za dunia

  2. Bahari ni yake ndiye aliyeumba na mikono yake ilituumba sisi

  3. Bwana ametamalaki mataifa yatetema, ameketi juu ya makerubi mbinguni

  4. Yeye Bwana katika sayuni ni mkuu, katukuka juu ya mataifa yote.

  5. Mshangilieni Bwana, mwimbieni na zaburi, vinanda na baragumu vyote mvipige

  6. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa kuwa fadhili zake ni za milele

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page