top of page

Mshukuruni Bwana

Mshukuruni Bwana (Bwana Bwana), mshukuruni Bwana (Bwana) Bwana kwa kuwa ni mwema (Kwa maana fadhili zake ni za milele x2.

  1. Yeye ni Mungu wa miungu, yeye ni Bwana wa mabwana (Yeye peke yake amefanya maajabu makuu x2).

  2. Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake (Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji x2

  3. Yeye aliyefanya mianga jua litawale mchana (mwezi nazo nyota zitawale usiku x2

  4. Yeye aliyetukumbuka katika unyonge wetu (akatuokoa na watesi wetu x2).

  5. Yeye anakipatia kila chenye mwili chakula (mshukuruni Mungu – wa mbingu kwa maana ni mwema x2

8 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page