top of page

Ni nani aliye Mungu, Mungu ila Bwana Ni nani aliye mwamba, mwamba ila Mungu (Ni Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu aha! ni Mungu ndiye kimbilio la unyonge wangu aha! Naye anaifanya kamilifu njia yangu) x2

  1. Ni yeye Bwana aliye nguvu zangu nampenda sana, ni yeye Jabali langu na boma langu na Mwokozi wangu Mungu wangu mwamba wangu ninayemkimbilia ngao yangu na pembe ya wokovu wangu na ngome yangu

  2. Katika shida zangu nilimwita Bwana ee Bwana Na kumlalamikia Mungu ee Mungu akaisikia sauti yangu hekaluni mwake kilio changu kikaingia masikioni mwake

  3. Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu akanilipa sawasawa na haki yangu nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa hivyo nitaokoka na adui zangu

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page