top of page

Mpenzi wa Moyo

Ninakupenda, ewe Mwokozi wangu, rafiki yangu, penzi wa moyo wangu. Ukae nami daima ndani yangu, nipate nguvu na heri siku zote x 2.

  1. Nina kutolea mwili na roho yangu, unipe rehema zako nipate nguvu. Nikae nikupendeze Mwokozi wangu, shetani mwovu kamwe asinipate.

  2. Nilinde niwe imara na mwenye nguvu, nisitumbukie tena katika dhambi. Unioshe yaliyo ya heri kweli, nipate kuishi kwa kupendeza Bwana.

  3. Wewe uliye njia kweli na uzima, niongoze vema daima siku zote. Uniangazie mwanga palipo giza, nifike kwa Mungu Baba kwa njiia zake.

  4. Nakukaribisha Bwana moyoni mwangu, nijalie baraka zako ewe Bwana. Hata siku ya mwisho itakapo wadia, niite mbinguni kwenye heri milele.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page