top of page

Mpeni Mungu Mali Yake

Mpeni Mungu mali yake,Mpeni Bwana haki yake x2

Leteni zawadi kwa Bwana-

Mkate kiini cha ngano -

Divai tunda la mzabibu -.

Na Bwana atavipokea -


Na kazi za mikono yetu -

Nazo nafaka za mashamba

Nayo mapato ya mashamba

Na Bwana atayatakasa –


Sisi ni mali yake Bwana -

Toeni nafsi kwake Bwana –

Nayo furaha na uchungu

Na Bwana atavipokea –


Vitu vyote mali ya Bwana

Itangazeni sifa yake –

Uhubirini ukuu wake -

Milele hata na milele –

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page