top of page

Moyo Wangu Wamuadhimisha

Moyo wangu wamuadhimisha Wamuadhimisha Bwana, na roho, roho yangu, Roho yangu yashangilia, (shangilia)

yashangilia, Roho yangu yashangilia, katika Mungu wangu


Kwa kuwa amemuangalia kwa huruma

mtumishi wake, tangu sasa vizazi vyote,

wataniita mwenye heri kwani yeye aliye

Mwenyezi amenitendea mambo makuu

Jina lake ni takatifu, jina lake ni takatifu


Huruma yake ni kwa wote kwa wale

wote wamchao kizazi hata na kizazi,

kizazi hata na kizazi x2


Amewaondosha wenye enzi, kutoka kwa

kiti cha enzi, kawakuza wanyenyekevu,

kawakuza wanyenyekevu. Amewashibisha

wenye njaa, amewashibisha na mema

matajiri kawarudishi, rudisha mikono

mitupu


Amempokea mtumishi wake, mtumishi

wake Israeli, kama alivyowaambia,

waambia mababu zetu mababu zetu

Ibrahim, Ibrahim wa wazao wake milele

hata na milele, milele hata na milele


Atukuzwe ee Mungu Baba, atukuzwe

na Mungu Mwana naye Roho Mtakatifu,

naye Roho Mtakatifu kama mwanzo na

siku zote, siku hata milele. Siku zote hata

milele, siku zote hata milele

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page