top of page

Moyo wako Mpendelevu

Moyo wako, Yesu mpendelevu, watuhurumia masikini;

Wawapokelea wakosefu, kwa msamaha, wema na amani.

Moyo hazina ya neema, utujalie daima!

Yesu twasalimu wako Moyo, twakushukuru kwa mapenziyo


Moyo makimbilio salama, takujalia japo wadhambi;

Tupokee leo kwa huruma, kasikilie yetu maombi!

Yesu utuhurumie, kwa wema tufanyizie,

Twataka kukutii daima, na kwako kupata usalama


Moyo ukashibishwa huzuni, kwa kutustahilia huzuni msamaha

Pia ukatiwa msalabani wa mbingu utupatie raha

Tufundishe leo pia, kukupenda kuzidia;

Donda lako utufungulie, kwako milele tukimbilie

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page