top of page

Misa Cosmas

Bwana, Bwana utuhurumie x2

Ee Bwana x5 tuhurumie x2

Bwana utuhurumie, Bwana,

Bwana utuhurumie x2

Ee Bwana, Bwana, Bwana Ee Bwana,

Ee Bwana, Ee Bwana utuhurumie x2


Kristu (all as above) xx

Bwana (all as above)x2


UTUKUFU

Utukufu kwa Mungu x2,

na amani duniani x2, kwa watu wenye

mapenzi (kwa watu wenye),

kwa wenye mapenzi mema.


Tunakusifu Bwana, tunakuheshimu

Twakuabudu Bwana, tunakutukuza

Twakushukuru Baba Mwenyezi, Mfalme wa Mbinguni


Ee Bwana Yesu Kristu Mwana wa pekee

Mwana kondoo wa Mungu, Mwana wake Baba

Uondoaye makosa yetu utuhurumie


Tunakusihi Bwana utusikilize

Wewe unayeketi kuume kwa Baba

Ni peke Bwana ni Mtakatifu mkuu Yesu Kristu


Pamoja naye Mungu Roho Mtakatifu

Katika utukufu wake Mungu Baba

Milele yote, milele yote, Amina. Amina.


NASADIKI

Ninasadiki Kwa Mungu, Nasadiki, nasadiki

Ninasadiki kwa Mungu (kweli) nasadiki x2


Nasadiki kwa Mungu Baba,

Muumba wa Vyote,

anayetawala milele


Nasadiki Mwanaye Yesu,

Mwana wa Mungu;

Mwana wa Maria, Mkombozi wetu


Alitufia sadaka yetu;

Akafufuka siku ya tatu,

akapaa mbinguni


Amekaa kuume kwa Baba,

atarudi siku ya mwisho

Kuwahukumu wazima na wafu


Nasadiki kwa Roho Mtakatifu na kanisa Katoliki

Tulipobatizwa, tukapewa uzima wa Mungu

Tukaondolewa dbambi zetu


Tutafufuka mwili na roho;

na kuishi na Mungu milele, milele Amina


MTAKATIFU

Mtakatifu Bwana

Mtakatifu,

mtakatifu Mungu wa majeshi x2

Mbingu na dunia zimejaa

Utukufu wako zimejaa

Zimejaa, zimejaa utukufu wako


Hosana Hosana

kwa Mwana wa Daudi

Hosana, Hosana kwa Mwana wa Daudi

Hosana, Hosana;

Hosana juu mbinguni

Hosana, Hosana, Hosana juu mnbinguni


Mbarikiwa yeye mwenye kuja

Kwa jina la Bwana mwenye kuja

Mbarikiwa mwenye kuja

kwa jina la Bwana


Hosana Hosana

kwa Mwana wa Daudi

Hosana, Hosana kwa Mwana wa Daudi

Hosana, Hosana;

Hosana juu mbinguni

Hosana, Hosana, Hosana juu mnbinguni



BABA YETU

Baba yetu uliye mbinguniJina lako litukuzwe ufalme wako ufike


Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni utupe leo mkate wetu wa kila siku


utusamehe makosa yetu kama tunavyo wasamehe sisi

waliotukosea

usitutie katika kishawishi lakini utuopoe maovuni


kwa kuwa ufalme ni wako nazo nguvu ni zako, na utukufu hata milele.


MWANA KONDOO

Mwana kondoo wa Mungu tuhurumie x2

Uondoaye dhambi zetu tuhurumie x2


Mwana kondoo wa Mungu tupe amani x2

Uondoaye dhambi zetu tupe amani x2

Utupe amani Ee Bwana utupe amani x2

Utupe amani Ee Bwana utupe amani x2

25 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page