top of page

Mimi Nimewatangulia

Mimi nimewatangulia x2 Kwenda mji wa Galilaya x2 nendeni mkawaambie mitume wangu hivyo x2

  1. Wale akina mama wakaondoka mapema, kumpaka mafuta ya kuutunza mwili, na kwa hofu yao kaburi liko wazi, wakarudi haraka kuwaambia mitume.

  2. Malaika wawili mle kaburini, walimwambia Maria binti usiogope, amefufuka mapema jinsi alivyosema, mjini Galilaya amewatangulia.

  3. Ndipo Yesu akasema nendeni ulimwenguni, mkafanye wafuasi wangu pande zote, mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana, na la Roho wa kweli mimi nimewatangulia.

  4. Sitawaacha yatima narudi kwa Baba yangu, kutayarisha makao huko juu mbinguni nitamtuma mlinzi awe nanyi nyote, ndiye Roho wa Mungu Roho Mtakatifu.

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page