top of page

Mimi ndimi Chakula

(Mimi ndimi chakula) chakula cha uzima (mimi ni nuru ya ulimwengu, mimi, ndimi njia ya uzima,mimi ndimi mchungaji mwema mimi ndimi mzabibu) x2

1. Msipokula huu mwili wangu, hamna uzima ndani yenu, msipokunywa hii damu yangu hamtapata uhai ,kuleni mwili wangu , kunyweni damu yangu mpate ishi milele.

2. Naye alikuwa naye hatakwenda gizani, bali atakuwa na uzima na nuru ya uzima, mtu haji kwake Baba ila kwa njia yangu ,nifuateni tufike mbinguni.

3. Ninawajuwa kondoo wangu na kondoo nao wanijuwa ,huisikia sauti yangu kondoo hunifuata ninawapa malisho ,malisho yale mema malisho ya mbinguni.

4. Baba ndiye mkulima ,ninyi ndinyi matawi ,ninyi ni matawi ya mzabibu huu,tawi lisilozaa Baba analiondoa, tawi lizaalo analitunza .

5 views0 comments

Comentarios

Obtuvo 0 de 5 estrellas.
Aún no hay calificaciones

Agrega una calificación
bottom of page