top of page

Millenium Mass


Bwana Bwana Bwana utuhurumie x2

Kristu Kristu (Kristu) utuhurumie x2

Bwana…………………


UTUKUFU

SA Utukufu kwa Mungu juu mbinguni

TB Na amani kote duniani

ALL Kwa watu wa mapenzi mema

Tunakusifu tunakuheshimu ,Tunkuabudu tunakutukuza x2

2. Twakushukuru Mungu kwa ajili,Ya utukufu wako mkuu ee Bwana,Ni wewe Mungu Mfalme wa mbinguni.

3. Baba Mwenyezi Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee Mwana wa Baba,Mwana Kondoo Mwana wake Mungu.

4. Uondoaye dhambi za dunia,Utuhurumie tuhurumie,Maombi yetu Baba upokee.

5. Uketiye kuume kwake Baba, Utuhurumie tuhurumie, Ni wewe peke peke Mtakatifu.

6. Pekee yako Bwana pekee mkuu, Ewe Yesu Kristu pamoja naye,Roho Mtakatifu milele yote.`


NASADIKI- MILLENIUM

1. S/A- Nasadiki kwa Mungu mmoja- Nasadiki

T/B- Ndiye Baba yetu mwenyezi - Nasadiki

S/A- Muumba mbingu pia dunia - Nasadiki

T/B- Nasadiki kwa Yesu Kristu - Nasadiki (kweli)


Nasadiki, nasadiki ninasadiki x2


2. Mwana wa pekee wa Mungu

Aliyezaliwa kwa Baba

Akapata mwili kwa Roho

Kazaliwa naye Bikira

3. Kisha yeye kasulubiwa

Kwa amri yake Pilato

Kwa ajili yetu kateswa

Akafa na akazikwa

4 Kafufuka katika wafu

Akapaa juu mbinguni

Ameketi kuume kwake

Mungu Baba yetu mwenyezi

5. Ndipo atakapotokea

Kuhukumu wazima na wafu

Kwake Roho Mtakatifu

Kwa kanisa la Katoliki

6. Ushirika wa watakatifu

Ondoleo ya dhambi zetu

Nangojea ufufuko wa miili

Na uzima wa milele


MTAKATIFU : MILLENIUM

(Mtakatifu) Bwana Mtakatifu Bwana Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi

(Mbingu na du)nia mbingu na dunia Zimajaa utukufu wako

Hossana juu x3 Mbinguni x2

Mbarikiwa) yeye x2 yule mwenye kuja Kwa jina la Bwana x2

AMINA

Amina Amina Amina x2.


BABA YETU

Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe Ufalme wako utufikie utakalo lifanyike x2

1. Duniani kama mbinguni- Jina lako litukuzwe

Tupe leo mkate wetu

Mkate wetu wa kila siku


2.Tusamehe makosa yetu-

Kama vile twawasamehe

Wale waliotukosea


3. Situtie kishawishini

Walakini utuopoe

Maovuni utuopoe


4. Kwa kuwa ufalme ni wako-

Nguvu na utukufu pia

Utukufu hata milele

57 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page