top of page

Military Mass

Tunakuomba ewe Bwana – utuhurumie sisi wakosefu utuhurumie x2

Tunakuomba ewe Kristu – utuhurumie x2

Dhambi tunatubu utuhurumie x2

Tunakuomba ewe Bwana……x2


UTUKUFU.

Utukufu kwa Mungu mbinguni na amani duniani kote (kwao wenye mapenzi mema)

  1. Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu, tunakutukuza.

  2. Twakushukuru mwenye utukufu, mfalme wa mbingu, Mungu Baba yetu.

  3. Ee Bwana Yesu, Mwana wa pekee, uliye mwana, Kondoo wa Mungu.

  4. Mwenye kufuta dhambi za dunia, ‘tuhurumie, utusikilize.

  5. Unayeketi, kuume kwa Baba, peke yako mkuu: Ee Yesu Kristu.

  6. Pamoja naye, Roho Mtakatifu, katika ‘tukufu wake Mungu Baba.


NASADIKI.

Ninasadiki:- mimi nasadiki,kweli nasadiki – mimi nasadiki.

Ninasadiki kwa Mungu mmoja – mimi nasadiki:

1. Baba mwenyezi muumba wa vyote – mimi nasadiki:

Na Yesu Kristu Mwanaye wa pekee – mimi nasadiki

Mwana wa Baba pia Bwana wetu – mimi nasadiki.


2. Baba mwenyezi muumba wa vyote – mimi nasadiki:

Na Yesu Kristu Mwanaye wa pekee – mimi nasadiki

Mwana wa Baba pia Bwana wetu – mimi nasadiki.


3. Aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu… akazaliwa

na yeye Bikira…na akateswa kwa

Ponsyo Pilato …. Kasulubiwa akafa, ‘kazikwa


4. Akashukiwa katika kuzimu… siku ya tatu

na akafufuka… akafufuka kutoka kwa wafu…

kapaa mbinguni kwa Baba Mwenyezi….


5. Yeye ‘kaketi kuume kwa Baba… na akakuja na

Ninasadiki kwa Roho mtakatifu…


6. Pia kanisa takatifu katoliki….na ushirika wa watakatifu….

maendeleo ya dhambi nasadiki… Na ufufuko wa miili

nasadiki… Na kwa uzima wa milele amina.



MTAKATIFU.

Mtakatifu mtakatifu – Mtakatifu ewe Bwana,

(Bwana wetu Mungu wa majeshi x2).

Mbingu na dunia zimejaa utukufu,

kweli zimejaa wako utukufu.

Hosanna – hosanna:- Hosanna x2. Juu mbinguni x2.

Amebarikiwa a-ajaye kwa jina, ajaye kwa jina, kwa jina la Bwana.


BABA YETU.

Baba yetu – ee Baba uliye mbinguni jina lako ee Baba litukuzwe.

1.Ufalme wako ufike utakalo lifanyike – jina lako

ee Baba litukuzwe. Duniani kama mbinguni

utakalo lifanyike – jina lako ee Baba litukuzwe.

2.Utupe leo mkate, mkate wa kila siku…

makosa utusamehe, tufanyavyo ndugu zetu….

3. Usitutie ee Baba, katika majaribu…

lakini utuopoe maovuni tuopoe…

4. Kwa kuwa ‘falme ni wako na nguvu na utukufu…

na nguvu na utukufu ‘tukufu hata milele…


MWANA KONDOO.

Mwana Kondoo wa – Mungu uondoaye dhambi za dunia – utuhurumie x2.

Mwana Kondoo wa – Mungu uondoaye dhambi za dunia – (tupe amani x3)

8 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page