top of page

Mfalme wa Amani

1. Mfalme wa amani mpeni heshima, Yerusalem mjini anaingia, na unyenyekeo na upole mkuu, anapanda punda Mwana wa Mungu.

Hosana juu! Hosana ju! Hosana juu.x2

2. Njoni mahebruni njoni watoto, leteni matawi ya kumsalimu, Mwana wa Daudi kweli Masiya, anakuja kwenu mwenye huruma.

3. Tandikeni nguo miguuni pake, Imbeni zaburi na mshangilie, mbarikiwa huyu ajaye kwetu, Kwa jina la Bwana Mkombozi mkuu.

4. Ufurahi sana we Yerusalem! yule wamwabudu roho za Mbingu, na huruma pole ana akujia, haki na amani, akuletea.

5. Ndimi za wachanga zafumbulia, kwa mwujiza sifa yake Masiya, na makundi yote ya malaika,

sifa na heshima, wanamtolea.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page