top of page

Mchunga Wangu

Mchunga wangu ameniandalia mema yote.

  1. Bwana ndiye mwenye kuchunga uzima wangu, na malisho yake kwangu ni raha kamili.

  2. Malishoni mwake mabichi ananilaza, sitakosa kamwe wala sitapungukiwa.

  3. Penye maji yale mazuri ya utulivu, ndipo kweli Mungu anaponiburudisha.

  4. Ananiongoza pasipo mashaka yeye, penye njia zake nzuri, adili na nyofu.

  5. Katika mabonde ya uvuli wa mauti, na(a)m ninapopita, sitaogopa mabaya.

  6. Kwa maana wewe upo pamoja na mimi,gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

  7. Waniandalia vitamu mezani mwako, nami nitashiba mbele za watesi wangu.

  8. Na kichwani pangu mafuta ukanipaka, na kikombe changu kweli chajaa memayo.

39 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page