top of page

Mbegu Zingine


Mbegu nyingine zikaanguka Mbegu nyingine (zikaanguka) Mbegu nyingine zikaanguka penye udongo mzuri! x2 Zikamea, zikamea na tena zikazaa x2

  1. Umeijalia nchi na kuistawisha, Mto wako Bwana umejaa maji mazuri

  2. Wewe unawaruzuku watu wote nafaka, Na umeuvika mwaka taji ya wema wako

  3. Pia na matuta yake maji umeyajaza, Wapasawazisha popote palipoinuka

  4. Wailainisha nchi kwa manyunyu ee Bwana, Hata na mimea yake wewe waibariki

  5. Kila upitapo kweli pamejaa unono, Huyadondokeza na malisho yote nyikani

  6. Na vilima vyote vajifunga nayo furaha, Na malisho yote yamevikwa nao kondoo



3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page