top of page

Maria Hoyee


1. Ya mgambo ikilia kweli kuna jambo hivyo msishangae ndugu zetu wapendwa, sisi leo tunaimba pia tunacheza tunazitaja sifa zake Mama Maria x2


Maria hoyee Mama Maria hoyee, kwa kazi nzuri ile uliyofanya, mfano wako kweli mfano bora, Maria hoyee Mama Maria hoyee x2


2. Ulitunza ubikira kwa mchumba wako ukajiweka vyema kwa ndoa ya baadaye, mfano kwao vijana wa kizazi hiki wenye madhumuni ya kuishiriki ndoa x2


3. Ulikubali kupata mimba yake Yesu, mpango wake Mungu uweze kutimia, ukamlea vizuri Mwana wake Mungu kwa maadili mema kama mzazi wake x2.


4. Herode alipotaka kumuua Yesu, wewe naye Yusufu mlikata kauli, uamuzi wa busara, mkamtorosha mlivyo shauriwa na sauti ya Mungu x2


5. Salamu Mama Maria umejaa neema, Bwana yu kweli nawe na umebarikiwa, mzao wa tumbo lako amebarikiwa watuombea kwake kweli unatupenda x2.

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page