top of page

Maneno saba ya Msalabani

Natumwimbie, Mwana Kondoo msalabani, na tumwimbie kwani aishi milele x 2

  1. Maneno saba ya msalabani, inafaa sana tuyafuate, Mwokozi aliyanena mwenyewe alipokuwa msalabani.

  2. Walipofika pafuvu la kichwa, wakamsulubu na wahalifu, neno lake la kwanza ndilo Bwana, wasamehe hawajui watendalo.

  3. Mwana alipo mwona mama yake, akamkabidhi kwa wanafunzi, mama tazama huyu mwana wako, nawe tazama mama yako huyo.

  4. Mhalifu huyo alimuomba, amkumbuke kwenye ufalme, amini leo hivi utakuwa, na mimi mjini huko peponi.

  5. Ilipotimia saa ya sita, akapaza sauti akilia, Eli, eli lama sabakithani, Mungu wangu mbona ueniacha.

  6. Hapo msalabani alikaa, kwa ukombozi wa dunia hii, akasema kuwa “naona kiu” “ili andiko lipate timia”

  7. Alichukua mzigo, mzito, hukumu ya dunia ya maasi, akatimiza yaliyomleta akasema ya kwamba; imekwisha.

  8. Giza la saa sita hadi tisa, kweli kitambaa kilipasuka, akalia Ee Baba mikononi, mwako nina iweka Roho yangu.

5 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page