top of page

Mama wa Msalaba

Yesu ananipenda hataki kunificha ukweli, tazama huyu Mama, huyu ndiye Mama yako.

Pale msalabani alitamka bila kusita, tazama huyu ndiye Mama, huyu ndiye Mama yako

Ninaringa ninaye Mama niliyepewa na Yesu, najivunia mimi na Yesu ni watoto wa mama mmoja, Bikira Maria, nampenda siku zote, Mama wa Msalaba, nampenda siku zote x2


Nikiwa kwenye shida sitatapatapa ovyo ovyo…….

Nitamwendea Mama, anayenijali siku zote…….


Sitakata tama kwa jambo lolote la dunia…….

Nina nguvu ya Yesu kwani ninaye Mama Maria…….


Watu wa ulimwengu, njoni tufaidi pamoja……

Acheni ukaidi jina Maria lina uwezo….


Saa ya kufa kwangu, Mama Maria hatanitupa…..

Atanisalimisha mikononi mwa Kristu mshinda…..

4 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page