top of page

Mama Maria

Maria Maria Mama wa rehema sisi wanao twakuja kwako, wewe uliye tegemeo letu twakulilia utusikie, wewe ni mama mwaminifu mama mpole mama wa Mungu na kanisa lote x2


Wewe ni Mama wa shauri njema mama mpole tuombee kwa mwanao mkombozi wetu


Mama Maria kimbilio letu na kinga yetu pia yeye ni tulizo letu wanadamu


Una Baraka kutoka kwa Mungu naye Yesu mwana wako amebarikiwa


Sisi wanao tunakulilia tunakusihi sala zetu zifikishe kwa mwanao Yesu


Ulikingiwa dhambi ya asili ukamzaa mkombozi wa dunia Bwana Yesu Kristu.

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page