top of page

Malkia wa Rozari

Mama Maria (Mama) Mama Maria mkingiwa dhambi ya asili, utuombee (Mama) tufike mbinguni Mama Maria x2

  1. Uliye teuliwa naye Mungu kuwa Mama yake, na kwa Roho kapata Mwana Yesu kitoto cha mbingu, kwa malezi yako bora nchi ilikombolewa, kesha kapalizwa na kuwekwa Malkia wa mbinguUtuombee kwa Mwanao tufike kwake.

  2. Uliye watokea Francisi, Lucia, Jacinta, kahimiza tusali rozari tupate amani, na kwa ajili ya wakosefu was’o na muombezi, na wale was’o mwamini Yesu ili waokoke tuombee kwa Mwanao tufike kwake.

  3. Changamoto za maisha zazidi kutulemea, zatikisa hadi Imani yetu sisi wanao, sikiliza nyimbo nzuri Mama tunakuimbiya, Malkia wa rozari Mama Mtakatifu wetu - Utuombee kwa Mwanao tufike kwake

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page