top of page

Malaika Kaleta Noeli

Malaika kaleta Noeli ya kwanza, Kwa wachunga kondoo katika makonde, Bethlehemu wakawa walinzi wa zamu, Wakaona usiku ajabu ya nuru

Noeli, Noeli, Noeli, Noeli, Yesu yu Mungu na binadamu x2


Wakaona mbinguni, mwangaza wa nyota, Ing'aayo kwa mbali na masharikini, Wakaenda upesi, walivyoambiwa. Bethlehemu wamwone Mwokozi horini


Mashariki watoka wafalme watatu, Mamajusi waliotafuta mfalme, Wafuata hii nyota waliyoiona, Wasipate kumkosa wanayemtafuta


Kiongozi ni nyota iliyowaleta Hata mji wa Daudi alimozaliwa Ikakaa mara moja isiendelee Pale pale nyumbani alimo Mwokozi


Mamajusi walipoingia nyumbani Wakapiga magoti kwa heshima kuu Mara hiyo walipozifungua hazina Manemane, uvumba, dhahabu, watoa


Basi sisi wakristu na tumsujudie Tumhimidi Mwokozi, aliyeviumba Vitu vyote mbinguni duniani na sisi Na ametufia na kutukomboa

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page