top of page

Maajabu ya Mungu

Maajabu ya Mungu

kaumba watu wa rangi mbalimbali x4

Wengine ni weusi, wengine ni weupe,

Wengine ni wekunde, wengine ni wekundu,

Wote ni wa Mungu, wote


Maajabu ya Mungu

kaumba watu wa kimo mbalimbali

Wengine ni warefu wengine ni wafupi,

Wengine ni wanene, wengine ni wembamba

Wote ni wa Mungu, wote


Maajabu ya Mungu

kaumba watu wa wito mbalimbali

Wengine ni wa ndoa, wengine ni watawa,

Wengine makuhani, wengine ni wa ndoa

Wote ni wa Mungu, wote


Maajabu ya Mungu

kaumba watu wa kazi mbalimbali

Wengine makarani, wengine ni polisi

Wengine ni waalimu, wengine mabalozi

Wote ni wa Mungu, wote


Maajabu ya Mungu

kaumba watu wa umri mbalimbali

Wengine ni watoto, wengine ni vijana,

Wengine ni wa kati, wengine ni wazee

Wote ni wa Mungu, wote


Maajabu ya Mungu

kaumba watu wa sifa mbalimbali

Wengine ni hekima, wengine ni busara,

Wengine polepole, wengine ni haraka

Wote ni wa Mungu, wote

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page