top of page

Lo! Kaburi Wazi


  1. Mama Maria tuambie, uliona nini njiani Nanyi mitume tueleze mliyemkuta pangoni (kweli) Ni malaika, toka mbinguni Tulimwona pale kaburini) x2

  2. Amefufuka ni hakika, amefufuka kweli kweli Dunia nzima ifurahi, hata mbinguni wanaimba ((kweli) Twimbe tucheze, twimbe turuke, Twimbe sana, twimbe aleluya) x2

  3. Nguvu za shetani kashinda, kamba za mauti amekata Ngome ya kuzimu kavunja, kaburi za wafu zafunguka ((kweli) Simba wa Yuda, amenguruma, Walinzi nao mbio watimua) x2

  4. Ameondoka kaburini, aelekea Galilaya Nasi twendeni hima hima, twendeni kule Galilaya((kweli) Twendeni leo, twendeni sote, Tumwimbie nyimbo za ushindi) x2

  5. Tumekombolewa kwa damu, damu yake Mwanakondoo Lango la mbingu liko wazi, kwao waliokombolewa ((kweli) Tukimwamini, tutaingia, Tutaishi na Mungu milele) x2

12 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page