top of page

Kwa Nyimbo Nzuri

Mataifa yote simameni mbele zake Bwana, Makabila yote njoni leo nazo ngoma zenu Chezeni mbele za Bwana! (Wajaluo na waimbe nyimbo Wamasai na waruke juu Wabaluhyia na wapige ngoma Wakikuyu na wacheze sana, Watu wote sisimukeni, Shangwe nderemo na kelele, pigeni makofi) x2


  1. Kwa nyimbo nzuri za furaha, njooni nyote mbele za Bwana Kwa shangwe na vigelegele, tumwimbie Mfalme wetu

  2. Vinanda vifijo kelele, makofi machezo nderemo Kusifu kweli kwawapasa, enyi wanyofu wa moyo

  3. Pigieni Mungu kelele, imbeni utukufu wake Tukuzeni sifa za Mungu, tangazeni matendo yake

  4. Shukuruni Bwana kwa zeze, kwa kinanda cha nyuzi kumi Mfanyieni Bwana shangwe, mtumikieni kwa furaha

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page