top of page

Kuimba Raha

Njoni enyi waumini njoni, (njoni), njoni tumsifu Bwana kwa nyimbo za shangwe x 2

Kuimba kuzuri sana – (Ni kuzuri) x 2 Nikiimba nyimbo nzuri namsifu Mungu wangu, naye anasikiliza sala zangu kwa njia ya nyimbo x 2. (Nitaimba tu, nitaimba tu, nitaimba siku zote nimsifu Mungu wangu) x 2

1. Njoni waumini, njoni tumsifu Mungu,

Njoni tumwimbie Mungu nyimbo za kusifu sasa – Njoo uimbe nasi.

Njoni waumini, njoni tumsifu Mungu,

Jina lake litukuzwe kwa nyimbo za shangwe, sasa njoo uimbe nasi.

Kuimba kuzuri sana……………………………..

2. Njoni ewe Baba, njoo ewe mama

Njoni tumwimbie Mungu nyimbo za kusifu sasa – Njoo uimbe nasi.

Njoo na vijana, njoni enyi watoto,

Njoni tumwimbie Mungu nyimbo za kumsifu, sasa njoni muimbe nasi.

Kuimba kuzuri sana……………………………..

3. Tangazeni pote, utukufu wa Mungu,

Njoni tutangaze sifa zake Mungu wetu, sasa – njoni muimbe nasi.

Pazeni sauti, pigeni vinanda,

Tumpigieni Mungu wetu kelele za shangwe, sasa njoni muimbe nasi

Kuimba kuzuri sana……………………………..

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page