top of page

Kristu ni Mfalme


Kristu ni mfalme wa mbingu na nchi, Kristu ni mfalme wa viumbe vyote (Astahili sifa, enzi na ukuu , na kuabudiwa daima milele) x2

  1. Mungu Baba alimwadhimisha Yesu Kristu akampa jina lipitalo kila jina, Kwa jina la Yesu kila goti litapigwa na ulimi utakiri kwamba Yesu ni Bwana

  2. Yesu Kristu atawala Kristu ni mfalme, na ufalme wake usio wa dunia hii, Ufalme wake ni wa mbinguni kwake Baba, atawala nyoyo zetu sote tumsujudie.

  3. Viumbe vyote vya uwinguni simameni, viumbe vya Ulimwenguni chezeni kwa shangwe. Furahini sana mbele zake mfalme wenu, Imbeni nyimbo za sifa msifuni mfalme.

  4. Sauti yake inasikika pande zote, ukipenda utashika amri zake Bwana, Yeye ndiye njia kweli ya kwenda mbinguni, Na uzima wetu umo mikononi mwake.

11 views0 comments

תגובות

דירוג של 0 מתוך 5 כוכבים
אין עדיין דירוגים

הוספת דירוג
bottom of page