top of page

Kristo wa Neema Zote

Kristo wa neema zote imbisha moyo wangu

Mifulizo ya Baraka inaamsha shangwe kuu.

Unifunze nikupende, nikuandame kote,

Moyo wangu ukajaefuraha na tumaini.


Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku.

Salama aniongoza hata kule nyuumbani.

Yesu alinitafuta njiani mbali kwake,

Akatoa damu yake nipone hatarini.


Kweli mimi mwiwa mkubwa wa neema daima;

Wema wako unifunge zaidi kwako Bwana.

Ili nisivutwe tena kukuacha, ee Mponya,

Nitwalie moyo wangu uwe wako kamili.

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page