top of page

Kiserian Mass

Utuhurumie

Bwana utuhurumie Ee Bwana x2

Bwana utuhurumie


Kristu utuhurumie Kristu utuhurumie x2,

(utuhurumie)


Bwana utuhurumie


UTUKUFU

Utukufu kwa Mungu juu mbinguni

na amani na amani Duniani Duniani kwa

kwa watu wenye mapenzi mema


Tunakusifu, tunakuheshimu,

twakuabudu, tunakutukuza

Twakushukuru, mfalme wa Mbinguni,

kwa ajili ya utukufu wako.


Ee bwana Mungu, Mfalme wa mbinguni,

Baba Mwenyezi, Muumba wa wote

Ee Bwana Yesu, Mwana wa pekee

Mwana kondoo, Mwana wake Mungu.


Uondoaye, dhambi za dunia,

tuhurumie, utuhurumie

Uondoaye, dhambi za dunia,

ulipokee, hili ombi letu.


Unayeketi kuume kwa Baba tuhurumie,

utuhurumie, Kwa kuwa wewe,

ndiwe peke yako, Mtakatifu,

peke yako Bwana


Peke yako mkuu, Bwana Yesu Kristu,

pamoja naye, Roho Mtakatifu

Kwa utukufu, wake Mungu Baba,

milele yote, Amina, Amina


NINASADIKI

Ninasadiki, ninasadiki, ninasadiki Ninasadiki, ninasadiki


Ninasadiki kwa Mungu mmoja, Baba mwenyezi muumba wa mbingu na vitu vinavyoonekana pia ambavyo

havionekani


Ninasadiki kwa Yesu Kristu,Mwana wa pekee

Mwana wake Mungu Mwanga kwa Mwanga na Mungu kweli,

Tangu milele atoka kwa Baba


Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba

Ambaye vitu vyote vimeumbwa naye, ameshuka toka mbinguni

Kwa ajili yetu sisi wanadamu, na kwa ajili ya wokovu wetu


Akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwake yeye

Bikira Maria akawa mwanadamu, akasulibiwa Pia kwa ajili yetu sisi, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato Akafa akazikwa


Akafufuka siku ya tatu kapaa mbinguni ilivyoandikwa Atarudi tena kwa utukufu kuwahukumuwazima na wafu


Ninasadiki pia kwa Roho, Mtakatifu, mleta uzima

Atokaye kwao Baba na Mwana, aliyenena, kwao manabii


Ninasadiki, kanisa moja, katoliki, hilo la mitume, Ninaungama na ubatizo, ufufuko na, uzima milele.


BABA YETU

Baba yetu uliye mbinguni Jinalo litukuzwe Baba yetu ufalme wako ufike (ewe Baba) Utusamehe makosa yetu Kama twawasemehe Baba na sisi wale watukoseao (ewe Baba)


Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni

Utupe leo mkate wetu Mkate wa kila siku


Situtie katika vishawishi, Baba yetu

Lakini utuopoe Tuopoe maovuni


Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu

Na nguvu utukufu Utukufu hata milele


MWANA KONDOO

Mwanakondoo (mwana) wa Mungu

Uondoaye dhambi za dunia Utuhurumie, utuhurumie

Mwana mwanakondoo wa Mungu

Mwana kondoo - Wa Mungu wake Mungu


Mwanakondoo wa Mwana kondoo wake Mungu

Uondoaye dhambi za dunia

Uondoaye dhambi, dhambi za dunia

Uondoaye dhambi za dunia

Utujalie amani.

30 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page