top of page

Kiserian Mass


BWANA UTUHURUMIE:

Utuhurumie Bwana utuhurumie

Bwana utuhurumie,

Bwana utuhurumie, Bwana utuhurumie


T/B: Kristu utuhurumie


ALL: Kristu utuhurumie


Utuhurumie Bwana utuhurumie

Bwana utuhurumie

Bwana utuhurumie, Bwana utuhurumie


UTUKUFU:

Utukufu kwa Mungu juu mbinguni , (na amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema) x 2


Ladies. Tunakusifu tunakuheshimu, twakuabudu tunakutukuza.

Men . Twakushukuru Mfalme wa mbinguni kwa ajili ya

utukufu wako.


Ladies. Ee Bwana Mungu Mfalme wa mbinguni Baba Mwenyezi Muumba wa vyote.

Men. Ee Bwana Yesu Mwana wa pekee Mwana Kondoo Mwana wake Mungu.


Ladies. Uondoaye dhambi za duniani, tuhurumie utuhurumie

Men. Uondoaye dhambi za dunia, ulipokee hili ombi letu.


Ladies. Unayeketi, kuume kwa Baba, tuhurumie, utuhurumie

Men . Kwa kuwa wewe, ndiye peke yako, Mtakatifu, peke yako Bwana


Ladies. Peke yako mkuu, Bwana Yesu Kristu pamoja naye Roho Mtakatifu

Men. Kwa utukufu, wake Mungu Baba, milele yote, Amina Amina.


NASADIKI

Ninasadiki – Nasadiki x3 Ninasadiki..ninasadiki, nasadiki… ninasadiki- nasadiki

Ninasadiki kwa Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, muumba wa mbingu, na vitu vinavyo onekana pia ambavyo havionekani.

Ninasadiki kwa Yesu Kristu, Mwana wa pekee, Mwana wake Mungu. Mwanga kwa Mwana na Mungu kweli, tangu milele atoka kwa Baba.

Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba ambaye vitu vyote vimeumbwa naye, ameshuka toka mbinguni, kwa ajili yetu sisi wanadamu, na kwa ajili ya wokovu wetu.

Akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwake yeye Bikira Maria akawa mwanadamu, akasulubiwa pia kwa ajili yetu sisi, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akafa akazikwa.

Akafufuka siku ya tatu, kapaa mbinguni ilivyoandikwa, atarudi tena kwa utukufu, kuwahukumu wazima na wafu.

Ninasadiki pia kwa Roho, Mtakatifu mleta uzima, Atokae kwa Baba na Mwana, aliyenena kwao manabii.

Ninasadiki kanisa moja, katoliki hilo la mitume, ninaungama na ubatizo, ufufufko na uzima milele.

81 views0 comments

コメント

5つ星のうち0と評価されています。
まだ評価がありません

評価を追加
bottom of page