top of page

Kipeperushe Kitambaa Chako

Jiangalie jinsi unavyoenenda, ujiulize kama hivyo ni sawa Ndugu rejea ahadi yako kumkataa Ibilisi muovu Dhamira yako inakuambia nini, inakusuta au bado ni huru, sasa

Ndugu rejea ahadi yako kumfuata Bwana Yesu milele

Ewe Mwenzangu - kipeperushe kitambaa chako Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta Kisichafuke - kipeperushe kitambaa chako Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta Kiweke safi - kipeperushe kitambaa chako Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta


Uliye naye kweli ni mzuri sana, pia kumbuka yuko wako wa ndoa - Uliyeapa ni wewe sio mwingine, kushikamana naye yule mmoja, basi -


Maendeleo kweli ni muhimu sana, lakini na wenzako wanahitaji - Hicho kipato ndicho ulichopimiwa, au mwenzetu unachota zaidi, leo -


Unatamani kuwa mwenye madaraka, umejiandaaje kuyatumia - Je ni halali watu tukakutukuza, wakati yupo yule alokuumba, haya -


Kumbuka Yesu alipigwa mijeredi, kwa sababu ya haya unayotenda - Akatundikwa mtini akiwa tupu, kadhalilishwa mwisho akauawa, hivyo -


Kumbuka kuwa siku ile inakuja, matendo yako yote kuhesabiwa - Ni heri leo ukitunze kitambaa, siku ya mwisho kiwa bado cheupe, kweli -

10 views0 comments

Comentarios

Obtuvo 0 de 5 estrellas.
Aún no hay calificaciones

Agrega una calificación
bottom of page