top of page

Kimya Bara na Bahari

Kimya bara na bahari, kimya mbingu na dunia Bwana na Muumba wenu, mtoto Yesu asinzia

Kimya, kimya, asinzia, mpenzi wetu mtoto Yesu x2


Amelazwa manyasini, mchanga mkiwa, myonge pia Yosefu na Maria wamo, mtoto Yesu kumtunzia


Malaika wanashuka, mfalme wao kumlindia Wanatunga nyimbo nzuri, mtoto Yesu kumwimbia


Wachungaji waja mbio, kwa mshangao waingia Waanguka magotini, mtoto Yesu kumuabudia


Nasi pia twende hima, Mungu wetu kumwangalia Twende sote kwa juhudi, mtoto Yesu kumwamkia

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page