top of page

Kariobangi Mass


BWANA UTUHURUMIE.

Utuhurumie Ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana

‘TuhurumieEe Bwana, ee Bwana, ee Bwana, Bwana, utuhurumie.


Utuhurumie, Ee Kristu


Utuhurumie, Ee Bwana


UTUKUFU

Utukufu juu kwa Mungu, utukufu juu mbinguni, na amani kote duniani kwa wenye mapenzi mema.


Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu,tunakutukuza, twakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu.


Ewe Mungu ndiwe Mfame, wa mbinguni Baba Mwenyezi, ewe Bwana Yesu Kristu, wa pekee mwana wa Baba.


Ewe Yesu Mwanakondoo, wa Mungu mwana wa Baba, ewe mwenye kuziondoa dhambi zetu tuhurumie.


Ewe mwenye kuziondoa, za dunia dhambi za watu, ewe mwenye rehema nyingi, upokee maombi yetu.


Uketiye kuume kwake, Mungu Baba tuhurumie, kwa kuwa ndiwe uliye, peke yako Mtakatifu.


Peke yako ni wewe Bwana, peke yako Bwana mkuu, peke yako ni Mkombozi, peke yako Yesu Kristu.


Naye Roho Mtakatifu, katika utukufu wake, Mungu mmoja anayeishi, na kutawala milele yote.


NASADIKI: KARIOBANGI

1. Nasadiki kwa Mungu mmoja - Ninasadiki

Ndiye Baba yetu Mwenyezi- Ninasadiki

Muumba mbingu pia dunia - Ninasadiki

Nasadiki kwa Yesu Kristu

Nasadiki, nasadiki, ninasadiki ,Nasadiki, nasadiki, ninasadiki.


Mwana wa pekee wa Mungu- Ninasadiki.

Mwenye kuzaliwa kwa Baba- Ninasadiki

Akapata mwili kwa Roho- Ninasadiki

Kazaliwa naye Bikira - Ninasadiki


Kisha yeye kasulubiwa – Ninasadiki

Kwa amri ya Ponsyo Pilato- Ninasadiki

Kwa ajili yetu kateswa- Ninasadiki

Akafa na akazikwa- Ninasadiki


‘Kafufuka katika wafu- Ninasadiki

Kapaa juu mbinguni- Ninasadiki

Ameketi kuume kwake- Ninasadiki

Mungu Baba yetu Mwenyezi


Ndipo atakapotokea- Ninasadiki

Kuhukumu wazima na wafu- Ninasadiki

Kwake Roho Mtakatifu - Ninasadiki

Kwa kanisa la Katoliki

Ushirika wa watakatifu- Ninasadiki

Ondoleo la dhambi zetu- Ninasadiki

Nangojea ufufuko wa mwili- Ninasadiki

Na uzima wa milele


MTAKATIFU: KARIOBANGI

Mtakatifu, Mtakatifu, mtakatifu, Bwana Mungu wa majeshi

Mbingu na dunia zimejaa ‘tukufu wako.


Hosana - Hosanna juu mbinguni}

Hosana - Hosana juu mbinguni}x2


Mbarikiwa - Anayekuja kwa jina lake Bwana Mungu x2


FUMBO LA IMANI; KARIOBANGI

V. Fumbo la Imani

W. Fumbo la Imani Kristu alikufa

Fumbo la Imani Kristu alifufuka

Kristu atakuja tena x2.


BABA YETU

Baba Yetu uliye mbinguni Jina lako litukuzwe, Ufalme wako ufike utakalo lifanyike x2


Duniani kama mbinguni

Tupe leo mkate wetu

Mkate wetu wa kila siku


Tusamehe makosa yetu

Kama vile twawasamehe

Walio tukosea sisi

Situtie majaribuni.

walakini utuopoe

maovuni utuopoe

Kwa kuwa ufalme ni wako

Na nguvu na utukufu

Utukufu hata milele


MWANA KONDOO

Ee Mwana Kondoo

Uondoaye dhambi za dunia utuhurumie

Ee Mwana Kondoo

Uondoaye dhambi za dunia utuhurumie

Ee Mwana Kondoo

Uondoaye dhambi za dunia utujalie amani.

11 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page