top of page

Kakamega Mass


Ee Bwana (‘tuhurumie), ee Bwana ‘tuhurumie Ee Bwana (‘tuhurumie), Ee Bwana ‘tuhurumie) x2


Kristu (‘tuhurumie), Kristu (‘tuhurumie),

Kristu (‘tuhurumie), Kristu ‘tuhurumie, Kristu

(‘tuhurumie), Kristu (‘tuhurumie), Kristu

(‘tuhurumie), Kristu ‘tuhurumie.


Ee Bwana (‘tuhurumie) ….] x2


Utukufu

(Tuna)kusifu Baba, (tunaku)heshimu Baba, (tunaku)abudu Baba, tunakutukuza x2

  1. (Utukufu kwa Mungu juu mbinguni) x2, nayo amani kote duniani, kwa watu wenye mapenzi mema.

  2. (Tunakushukuru kwa ajili) x2, ya utukufu wako mkuu, ee Bwana mfalme wa mbinguni.

  3. (Ewe Yesu Kristu Mwana wa pekee) x2 Bwana Mungu Mwana Kondoo, Mwana Kondoo wa Mungu Baba.

  4. (Mwenye kuondoa dhambi za dunia) x2, Ee Bwana utuhurumie, na upokee maombi yetu.

  5. (Ndiwe pekee yako mtakatifu) x2, pekee yako ni wewe Bwana, pekee yako mkuu Yesu Kristu.

  6. (Pamoja naye Roho Mtakatifu), katika huo utukufu, wa Mungu milele yote.


Alleluya

(Alleluya alleluia) x2. (Alleluya alleluya alleluya) x2


Nasadiki

Ninasadiki kwa Mungu mmoja – Ninasadiki sadiki.

Ndiye Baba yetu Mwenyezi – Ninasadiki.

Muumba mbingu pia dunia – Ninasadiki sadiki.

Ninasadiki kwa Yesu Kristu – Ninasadiki.


Ninasadiki, nasadiki, ninasadiki, nasadiki x2


Mwana wa pekee wa Mungu –

Aliyezaliwa kwa Baba –

Akapata mwili kwa Roho –

Akazaliwa naye Bikira –


Kisha yeye akasulibiwa –

Kwa amri ya Ponsyo Pilato –

Kwa ajili yetu akateswa –

Akafa na akazikwa –


Akafufuka katika wafu –

Akapaa juu mbinguni –

Ameketi kuume kwake –

Mungu Baba yetu Mwenyezi –


Ndipo atakapotokea –

Kuhukumu wazima na wafu –

Kwake Roho Mtakatifu –

Kwa Kanisa la katoliki –


Ushirika wa watakatifu –

Maondoleo ya dhambi zetu –

Nangojea ufufuko wa mwili –

Na uzima wa milele –


Mtakatifu

Mtakatifu we, mtakatifu mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi, mbingu na dunia (zimejaa) zimejaa kweli utukufu wako x2


[Hossana juu, hosanna, hosanna juu, hosanna juu mbinguni, (hossana juu) x3 mbinguni] x2


(Mbarikiwa yule anayekuja) kwa jina kwa jina la Bwana, Mbarikiwa yule) anayekuja kwa jina lake Bwana Mungu.

Fumbo La Imani

Tunatangaza fumbo la imani. [Yesu Kristu alikufa (Yesu), Yesu Kristu kafufuka (Yesu),

Yesu Kristu atakuja (Yesu), atakuja tena)] x2


Amina

Amina amina amina amina. (Amina amina amina) x2


Baba Yetu

(Baba yetu uliye mbinguni), jina lako litukuzwe, ufalme (Ee Baba) wako utufike (ee Baba), utakalo Baba lifanyike x2


  1. Utakalo Baba lifanyike, duniani kama mbinguni, tupe leo Baba mkate wetu, mkate wetu wa kila siku.

  2. Utusamehe makosa yetu, tusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe, waliotukosea nasi

  3. Usitutie majaribuni, situtie majaribuni, walakini utuopoe, maovuni utuopoe

  4. Kwa kuwa ufalme ni wako, ufalme ni wako Baba, na nguvu na utukufu, utukufu milele yote


Mwanakondoo

(Mwana) Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, Mwana Kondoo wa Mungu utuhurumie x2

(Mwana) Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, Mwana Kondoo wa Mungu tujalie amani (Utujalie) utujalie amani utujalie, (utujalie) utujalie amani] x2

73 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page