top of page

Kabila Langu



Kabila langu nimekukosea nini? au nimekusikitisha nini? nijibu.

1. Kwa kuwa nimekutoa katika nchi ya Misri, umemtayarishia Mkombozi wako msalaba.

2. Mimi nimekuongoza jangwani kwa miaka arobaini, nawe umemtayarishia Mkombozi wako msalaba.

3. Mimi nimekupanda kama shamba langu nzuri mno, nawe ukamchoma mkuki Mkombozi wako ubavuni

4. Mimi nimewapiga mijeledi wamisri kwa ajili yako, nawe ukanitoa nipigwe mijeledi.

5. Mimi nimekutoa Misri nikamtosa Faraho katika bahari ya Shamu, nawe ukanitoa kwa makuhani wakuu.

6. Mimi nimeifunua bahari mbele yako, nawe ukaufunua ubavu wangu kwa mkuki.

7. Mimi nimekuongoza mbele kwa nguo za wingu, nawe ukanipeleka mbele ya baraza ya Pilato.

8. Mimi nimekulisha mana jangwani, nawe ukanipiga makofi na mijeledi.

9. Mimi nikunywesha maji ya uzima toka mwambani, nawe ukaninywesha nyongo na siki.

10. Mimi nimewapiga wafalme wa Kaanani kwa ajili yako, nawe ukanipiga kichwa changu kwa mwanzi.

11. Mimi nimekupa fimbo ya kifalme, nawe ukanivika taji la miiba kiicwani.

12. Mimi nimekutukuza kwa uwezo mkubwa, nawe ukanitundika katika mti wa msalaba.

12 views0 comments

Comentários

Avaliado com 0 de 5 estrelas.
Ainda sem avaliações

Adicione uma avaliação
bottom of page