top of page

Johera (dakunyi's herahera) x2 Manyase endwaro wololo hawawene Johida (dakunyi's hidahida) x2 Manyase endwaro wololo niwakadhi njooni wote tushangilie, (Tuimbe kwa furaha, tucheze bila mwisho, tutoe shukrani kwa Bwana mtawala) x2

  1. Waumini simameni, mbele zake Mungu wetu Waimbaji mziimbe, sifa zake Jehova Rama Waumini tamkeni, utukufu wake Yahweh Makasisi na watawa na wacheze nyumbani mwake shangwe

  2. Kwa sauti ya kinanda, kwa filimbi na kayamba Kwa kinubi na kwa zeze, tunamwimbia Mungu wetu Kwa kelele za furaha, kwa makofi kwa machezo Kwa vigelegele kweli, njooni nyote tutoe shukrani

  3. Mwimbieni Mungu wetu, mwimbieni wimbo mpya Mwimbieni kwa furaha mwimbieni kwa shangwe kubwa Mungu wetu ni mkuu, ametenda maajabu Ameumba vitu vyote, ulimwengu na jeshi lake lote

  4. Mungu wetu katuumba, ili sote tumjue Sisi sote tumpende, tumtumikie daima Ametupa vitu vyote,atulinda siku zote Tuna heri ya milele, tutaishi mbinguni kwake Baba

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page