top of page

Jipe Moyo

Jipe moyo Bwana yuko nawe, (tena)

Hakuachi kamwe kwani yeye akupenda

Hata shida zikikuandama (ndugu)

Umtegemee, Yesu atakuongoza


Njia imejaa giza na umande, huku

watembea bila hata nuru wasi wasi hofu

yakujaa woga watawala wasimama

wima hujui pa kwenda ushujaa watoka

wabaki upweke, bali yu pamoja na wewe


Ndugu watoweka wakuacha pweke,

hata marafiki uliothamini watoroka, hofu

yakujaa woga watawala. Wasimama

wima hujui pa kwenda. Ushujaa watoka

wabaki upweke, bali yu pamoja na wewe


Kila utendacho, hakiwezekani, wajaribu

sana kufaulu wala hauwezi hofu yakujaa

woga watawala wasimama wima hujui

pa kwenda ushujaa watoka wabaki

upweke, Bali yu pamoja na wewe

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page