top of page

Itengenezeni Njia ya Bwana



(Itengenezeni njia ya Bwana, Bwana apite (mapito yake) Yanyoosheni mapito ya Mungu wetu aingie) x2

  1. Tazama namtuma mjumbe wangu, mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako, Sauti ya mtu(sauti ya mtu), aliaye nyikani nyikani inasema x2

  2. Ondoka ee Yerusalemu, usimame juu Tazama uione furaha, Inayokujia(inayokujia) inakuja kutoka kwake Mungu, Mungu wako x2

  3. Yajazeni yale mabonde yote yashusheni milima, Panyosheni na pale palipopotoka Tayarisheni (tayarisheni) tayarisha njia na mapito ya Bwana aingie x2

  4. Na watu wote wenye mwili, wataona wokovu, Wataona wokovu wake Mungu wetu, Kwa sababu (kwa sababu) yeye atakayetukujia ni mwokozi x2

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page