top of page

Yesu wa Vituko


  1. Huyu ndiye Yesu wa miujiza nauliza Huyu ndiye Yesu wa maajabu nauliza aliyegeuza maji kuwa divai Kwenye harusi kule Kana Galilaya

  2. Huyu ndiye Yesu Mnazareti nauliza Huyu ndiye Mwana wa seremala nauliza aliyewaita wavuvi wa samaki Akawageuza wavuvi wa watu

  3. Huyu ndiye Yesu mwenye huruma nauliza Huyu ndiye Yesu Simba wa Yuda nauliza aliyewakemea mapepo kwa nguvu Aliyewaamuru mapepo watoke

  4. Huyu ndiye Yesu mwenye baraka nauliza Huyu ndiye Yesu mwenye chakula nauliza, aliyewalisha watu elfu tano Kwa mikate mitano na samaki wawili

  5. Huyu ndiye Yesu mwenye vituko nauliza Huyu ndiye Yesu asiyeshindwa nauliza, aliyewatimua watu hekaluni Walipogeuza hekalu kuwa soko

  6. Huyu ndiye Yesu mwenye hekima nauliza Huyu ndiye Yesu mwenye elimu nauliza, aliyeng'amua hila zake shetani Pale nyikani alipojaribiwa

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page